Friday, August 28, 2020

TATIZO LA "UDATA" (TONGUE TIE)

Udata ni tatizo la kuzaliwa(congenital malformation) linalopelekea mtu kushindwa kutoa ulimi nje na kushindwa kuupandisha juu. Mara nyingi tatizo hilo huwakumba watoto wachanga zaidi. Tatizo hili kitaalamu huitwa Tongue tie /Ankyloglossia


    UDATA HUSABABISHWA NA NINI?

Kwa kawaida sehemu ya chini ya ulimi(Lingual frenulum) huwa inatengana na sakafu ya mdomo(floor of mouth) ili kuwezesha ulimi kufanya mjongeo ndani  na nje ya mdomo . Hivyo endapo utando huo wa chini wa ulimi ukashikana  na kuungana na sakafu ya mdomo hupelekea mtoto kupata "udata"/Ulimi kushikwa.(tongue-tie)




DALILI ZA UDATA KWA MTOTO MCHANGA

- Mtoto kushindwa kutoa ulimi nje au kuupandisha juu
-Mtoto kushindwa kunyonya vizuri maziwa ya mama
-Ulimi wa mtoto kuwa na umbo la moyo
-Mtoto mwenye udata pia hushindwa kumeza na hupelekea maradhi katika mfumo wa chakula
-Mtoto mwenye udata hushindwa kuzungumza/kuongea vizuri
(speech defect)


MATIBABU UDATA

Tatizo la udata linatibika kitaalam  hospitalini kwa kukata sehemu ya utando wa chini wa ulimi ulioungana na sakafu ya mdomo ili kuruhusu ulimi kufanya mjongeo ndani ya mdomo kitaalum inaitwh frenotomy.Hivyo mzazi ukigundua tatizo hili kwa mtoto muone daktari kwa ajili ya matibabu mazuri na ya usalama.


Tujifunze tena kwa undani kupitia video hii

    
   shukrani sana...Imeeandaliwa na 
Frank E Msuya
#DaktariJamii blogger
  
  Video source: Medicounter  Azam tv


5 comments:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Thanks Dr.Msuya for the information. Keep it upπŸ’ͺ🏾. Together we build a strong and healthy community!πŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎ

    ReplyDelete

TATIZO LA "UDATA" (TONGUE TIE)

Udata ni tatizo la kuzaliwa(congenital malformation) linalopelekea mtu kushindwa kutoa ulimi nje na kushindwa kuupandisha juu. Mara nyingi t...