UDATA HUSABABISHWA NA NINI?
Kwa kawaida sehemu ya chini ya ulimi(Lingual frenulum) huwa inatengana na sakafu ya mdomo(floor of mouth) ili kuwezesha ulimi kufanya mjongeo ndani na nje ya mdomo . Hivyo endapo utando huo wa chini wa ulimi ukashikana na kuungana na sakafu ya mdomo hupelekea mtoto kupata "udata"/Ulimi kushikwa.(tongue-tie)
DALILI ZA UDATA KWA MTOTO MCHANGA
- Mtoto kushindwa kutoa ulimi nje au kuupandisha juu
-Mtoto kushindwa kunyonya vizuri maziwa ya mama
-Ulimi wa mtoto kuwa na umbo la moyo
-Mtoto mwenye udata pia hushindwa kumeza na hupelekea maradhi katika mfumo wa chakula
-Mtoto mwenye udata hushindwa kuzungumza/kuongea vizuri
(speech defect)
MATIBABU UDATA
Tatizo la udata linatibika kitaalam hospitalini kwa kukata sehemu ya utando wa chini wa ulimi ulioungana na sakafu ya mdomo ili kuruhusu ulimi kufanya mjongeo ndani ya mdomo kitaalum inaitwh frenotomy.Hivyo mzazi ukigundua tatizo hili kwa mtoto muone daktari kwa ajili ya matibabu mazuri na ya usalama.
Tujifunze tena kwa undani kupitia video hii
shukrani sana...Imeeandaliwa na
Frank E Msuya
#DaktariJamii blogger
Video source: Medicounter Azam tv
Thank you for the knowledge
ReplyDeleteYou're warmly welcome
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteThanks Dr.Msuya for the information. Keep it upπͺπΎ. Together we build a strong and healthy community!ππΎππΎ
ReplyDeleteAmen... Together We canπͺπͺ
Delete